TAMKO LA KULAANI MAUAJI......CHAMA CHA WAZEE WANAUME TANZANIA (CCWWT)CHALAANI MAUAJI YA KIKATILI YA MTOTO MKOANI KAGERA

TAMKO LA (CCWWT) KULAANI MAUAJI YA KIKATILI YA MTOTO ASIMWE . Chama cha wazee wanaume Tanzaniaa (CCWWT)kimeungana na Rais Mh Dr Samia Suluhu Hassan na wadau wengine kulaani kitendo cha kuuawa kikatili kwa Mtoto Asimwe Novati mwenye ulemavu wa Ngozi (Albino) akiwa na umri wa miaka miwili na nusu yaliyotokea kijiji cha Gulamula Wilaya ya Muleba Mkoa wa Kagera Akitoa tamko hilo kwa niaba ya chama k iongozi mkuu wa chama hicho Bw Tadey Mchena amesema wanachama wa chama cha wazee wanaume kimesikitishwa sana na ukatili huo aliofanyiwa mtoto huyo na kuendelea kusisitiza umuhimu wa hatua kalia za kisheria kuchukuliwa kwa waliohusika. Aidha kwa mujibu wa Bw Mchena chama cha wazee wanaume Tanzania kiko tayari kutoa ushirikiano wa hali na mali ...