WANANCHI WANAOISHI JIRANI NA HIFADHI WATOBOA SIRI NZITO YA KUSHAMIRI KWA MIGOGORO KATI YAO NA WATENDAJI WA HIFADHI


 

Hivi karibuni mgogoro  wa  muda mrefu kati ya  wananchi  wa Kijiji cha Bugeri kilichoko wilayani  Karatu mkoani  Arusha na Hifadhi ya Taifa  ya  Ziwa  Manyara ulipata ufumbuzi baada ya serikali kuamua kumega eneo la ukubwa wa hekari nane (8) na kuligawa kwa wananchi waliokuwa wamelivamia ,

Taarifa ya uamuzi huo ilitolewa na mkuu  wa mkoa  wa Arusha Bw  John Mongela katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijjini hapo ambapo pia alitumia nafasi hiyo  kutoa  msimamo wa serikali.






Kikao hicho pia kiliwashirikisha watendaji wa hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara akiwemo mkuu wa hifadhi hiyo Kamishna wa Uhifadhi Eva Malya ambaye alielezea mchakato waliopitia hadi kufikia hatua.


pia  walikuwepo wataalam wa ardhi mkoa  wa Arusha walioongozwa na Mpima wa mkoa  Bw Dany Mruma ambaye alitoa  ufafanuzi wa kitaalam juu ya masuala ya mipaka na sheria zinazotumika.


baada ya maamuzi hayo wananchi nao wakapata nafasi ya kueleza mtazamo wao juu ya hatua hiyo na ndipo wakajikuta wakitoboa siri ya kuendelea  kushamiri kwa migogoro katika  maeneo yanayopakana na hifadhi.





Baada ya wananchi kutoboa siri  hiyo serikali nayo kupitia kwa mkuu wa mkoa Bw John Mongela ikaeleza msimamo  wake.

  //////////////// Kwa undani wa taarifa hii tembelea   AMTV upate habari kwa kina.////////////

                  ///////////////////////////////KARIBU  SANA ///////////////////////////////////

 

Comments

Popular posts from this blog

TAMKO LA KULAANI MAUAJI......CHAMA CHA WAZEE WANAUME TANZANIA (CCWWT)CHALAANI MAUAJI YA KIKATILI YA MTOTO MKOANI KAGERA

WAZIR PEMBE ATAKA UZINGATIAJI AFYA YA AKILI

VIONGOZI CHAMA CHA WAZEE WANAUME TANZANIA (CCWWT) WAPAZA SAUTI JUU YA HATUA ANAZOCHUKUA RAIS DR SAMIA