UTUNZAJI WA MAZINGIRA WAANZA KULETA TIJA WILAYANI LONGIGO KUPITIA BIASHARA YA HEWA UKAA


 

Wananchi  wa   vijiji  16  vya wilaya  ya Longido mkoani  Arusha wamesaini makubaliano ya kuanza kunufaika na hewa ukaa kati yao na wawekezaji  wa kampuni Soil for the Future Tanzania yanayoashiria  wananchi  hao kuanza  kunufaika  na  hewa ukaa  baada  ya  kuhifadhi mazingira  ambayo  yameanza  kuwavutia  wawekezaji hao wa  rasilimali  hiyo .


Wakizungumzia hatua hiyo viongozi na watendaji  wa vijiji  hivyo   wamesema tayari  wameshaingia  makubaliano  ya  awali ya miaka mitano  na wawekezaji  hao mbapo  kila  kijiji  kitapata  asilimia  51  ya  mapato  yatokanayo na hewa  ukaa  kila  mwaka. 



Hata hivyo  wananchi  hao  akiwemo Bw Simion Olotosoi  amewataka  wawekezaji hao kuheshimu makubaliano kwani uzoefu unaonyesha kwamba licha ya kuwepo kwa mikataba mingi ya uwekezaji asilimia kubwa haiwanufaishi wananchi kama  wanavyotarajia.

Kwa upande wake mwakilishi  wa  mwekezaji kutoka  kampuni  hiyo  ya Soil for the Future Tanzania Bw .Iddi Mfunda amewaondoa wananchi  hao hofu hiyo  kwa  kusema kuwa wakati  wa utekelezaji  wa mkataba huo  kampuni  itaendelea  kutoa  elimu kwa  wananchi  ya  namna bora ya kuendelea  kutunza  nyana  za  malishao  kwa  kuendesha ufugaji  unalinda mazingira



Katika  kuwahakikishia  wananchi  hao kuwa  mkataba huo  utatekelezwa  Makubaliano  ya wananchi  na  mwekezaji  huyo  yameshudiwa  na  mkuu  wa  wilaya  ya  Longido  Bw Marco Ngumbi  ambaye  pia ameendelea  kuwaondoa wananchi hao  hofu juu  ya mradi huo 

 Aidha Bw Ngumbi  amewataka  wananchi  wa vijiji vingine kuongeza  juhudi  ya  kutunza  mazingira  ili  kunufaika na  fursa  hiyo  ambayo pia  itaongeza malisho  ya  mifugo.

KWA  HABARI  ZAIDI FUATILIA   AMTV ,UZIPATE  KWA  KINA .

Comments

Popular posts from this blog

TAMKO LA KULAANI MAUAJI......CHAMA CHA WAZEE WANAUME TANZANIA (CCWWT)CHALAANI MAUAJI YA KIKATILI YA MTOTO MKOANI KAGERA

VIONGOZI CHAMA CHA WAZEE WANAUME TANZANIA (CCWWT) WAPAZA SAUTI JUU YA HATUA ANAZOCHUKUA RAIS DR SAMIA

TAMWA-ZANZIBAR YATOA RAI WAKATI WA UANDAAJI SERA, SHERIA