MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA TRA MKOA WA ARUSHA YATOA TUZO KWA WALIPAKODI, YAOMBA USHIRIKIANO ZAIDI
Watendaji wa Mamlaka
ya mapato nchini TRA mkoa wa Arusha wametoa Tuzo kwa baadhi
ya walipakodi katika hafla iliyofanyika
Mount Meru hoteli huku wakielezea mafanikio na baadhi ya changamoto
zinazoendelea kujitokeza katika
ukusanyaji wa Kodi ikiwemo biashara ya magendo
Wakiwa katika hafla hiyo mkurugenzi wa rasilimaliwatu na utawala wa wa malaka hiyo Bw Moshi Kabengwe alisema pamoja na kazi kubwa ya kukusanya kodi inayofanywa na watendaji wa mamlaka hiyo bado kuna tatizo kubwa la biashara ya magendo hasa katika maeneo ya mipakani .
Kutokana na hali hiyo Kabengwe amewaomba wananchi wa mikoa ya pembezoni ukiwemo wa Arusha kuunga mkono jitihada za kudhibiti biashara za magendo zinazofanywa na baadhi ya watu maeneo ya mipakani na watu wanaingiza na kutorosha bidhaa bila kulipa kodi .
Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni mkuu wa wilaya ya Arusha Bw Felician Mutahengerwa amewapongeza watendaji wa TRA kwa kujenga mahusiano mazuri na walipakodi na kupata mafanikio makubwa utaratibu ambao unafaa kuogwa na taasisi na idara zingine zikiwemo halmashauri..bw felisian mtahengerwa .
kwa mujibu wa watendaji wa TRA pamoja na changamoto zilizopo ushirikishaji na ushirikiano wanaopata kutoka kwa wananchi umewezesha kufikia na kuvuka malengo ya ukusanyaji wa kodi .
kwa undani zaidi wa habari hii tembelea AMTV...UPATE HABARI KWA KINA
Mwisho
.
Comments
Post a Comment