TAMKO LA KULAANI MAUAJI......CHAMA CHA WAZEE WANAUME TANZANIA (CCWWT)CHALAANI MAUAJI YA KIKATILI YA MTOTO MKOANI KAGERA
TAMKO LA (CCWWT) KULAANI MAUAJI
YA KIKATILI YA MTOTO
ASIMWE .
Chama cha wazee wanaume Tanzaniaa (CCWWT)kimeungana na Rais
Mh Dr Samia Suluhu Hassan na wadau wengine
kulaani kitendo cha kuuawa kikatili kwa Mtoto
Asimwe Novati mwenye ulemavu wa Ngozi (Albino) akiwa na umri
wa miaka miwili na nusu yaliyotokea kijiji cha Gulamula Wilaya ya Muleba Mkoa
wa Kagera
Akitoa tamko
hilo kwa niaba ya chama kiongozi mkuu
wa chama hicho Bw Tadey Mchena amesema wanachama wa chama cha wazee wanaume kimesikitishwa sana na ukatili huo aliofanyiwa mtoto huyo na kuendelea kusisitiza umuhimu wa hatua kalia
za kisheria kuchukuliwa kwa waliohusika.
Aidha kwa mujibu
wa Bw Mchena chama cha wazee wanaume Tanzania kiko
tayari kutoa ushirikiano wa hali na mali katika kukabili vitendo hivyo vya kikatili vinavyofanywa
na baadhi ya watu ambavyo kwa ujumla havikubaliki kwa namna yeyote,na
mahali popote Duniani na hata Mbinguni .
Sisi viongozi na wanachama wa CCWWT tunaungana na Mh Rais Dr Samia Suluhu hasan na wasaidizi wake akiwemo makamu wa Rais Mh Dr Philip Mpango ,Waziri Mkuu Mh Kasim Majaliwa ,Naibu Waziri Mkuu Mh Dr Dotto Biteko na Waziri wa maenndeleo ya Jamii jinsia na makundi maalum Mh Dorosi Gwajima kutoa pole kwa familia ndugu , na jamaa wa Marehemu Mtoto Asimwe Novati.
Aidha tunaiomba Jamii yote kwa ujumla kutokubali vitendo kama hivi kujitokeza katika maeneo yao na kuona umuhimu wa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola kuwadhibiti watu hawa wachache wanafanya vitendo hivi .
Na pia chama kinawaomba wazee wote wanaume popote walipo Tanzania bila kujali itikadi zao na tofauti zao za aina yeyote ile waungana na Mh Rais Dr Samia na wasaidizi wake katika kupambana na ukati huu kwani ni jambo linalowezekana.
Imetolewa na
Idara ya Habari na mawasiliano Chama cha wazee
wanaume Tanzania (CCWWT).
Comments
Post a Comment