VIONGOZI CHAMA CHA WAZEE WANAUME TANZANIA (CCWWT) WAPAZA SAUTI JUU YA HATUA ANAZOCHUKUA RAIS DR SAMIA
Viongozi wa Chama cha wazee wanaume Tanzania kinachoitwa (CCWWT) chenye makao yake makuu Jijini Arusha wametoa pongeza kwa Rais Dr Samia Suluhu Hassan kwa hatua anazoendelea kuchukua kwa watendaji wa serikali wanaokiuka sheria taratibu na maadili ya Uongozi
Miongoni mwa hatua zilizozungumziwa na viongozi wa chama hichi ni pamoja na ya kutengua uteuzi wa Naibu waziri wa katiba na sheria Mh Paulina Gekulu kwa kutuhumiwa kushiriki katika vitendo vinavyodaiwa kukiuka sheria suala ambalo wazee wanasema yeye kama kiongozi anayesimamia sheria hangepashwa kulifanya
Viongozi hao akiwemo mkuu wa CHAMA hicho Bw Tadei Mchena amesema Mh Rais Dr Samia Suluhu Hassan ameonyesha njia kwa vitendo ya uongozi unaosimamia utawala Bora .
"Kwa
niaba ya chama Cha wazee Wanaume Tanzania CCWWT tunamshukuru sana MH,Rais Dr
Samia Suluhu Hassan kwa hatua anazoendelea kuchukua dhidi ya viongozi
wanaoshindwa kukinda maadili ya majukumu waliopewa ambao kimsingi licha ya
kupiteza sifa ya kuwa viongozi wanaleta picha mbaya kwenye jamii.
Sisi kama wazee Wanaume Tanzania tunaunga mkono hatua hizi na tunamwambia Mh Rais aendeleze utararatibu huo kwani una tija KUBWA sana katika jamii na taifa kwa ujumla na pia tunamuahidi Mh Rais Dr Samia kwamba sisi chama Cha wazee Wanaume Tanzania tutamuunga mkono na tutatumia zetu na uwezo WETU kumsaidia .
Kwa Sasa tunajipanga kufanya ziara nchi nzima kutoa elimu kwa jamii Juu ya kusaidiana na serikali kupambana na vitendo vyote ukatili na ukiukwaji wa maadili vinavyoendelea kushika kasi na tumeshaanza hatua za awali za kutekeleza azma hiyo ikiwemo ya kukisanya nguvu.alisema Mchena Kiongozi mkuu wa Chama cha wazee wanaume Tanzania
Kiongozi
mwingine aliyezungumzia hatua hiyo ni pamona na ni Bw Michael Mwamaja ambaye ni Mweka hazina wa Chama yeye amesema anachokifanya
Mh Rais Dr Samia kwa Sasa ni moja na mambo ambayo watanzania wengi
wameyasubiri kwa muda mfefu .
Bw Michael Mwamaji amesema kinachomgusa zaidi juu ya maamuzi ya Dr Samia Suluhu Hassan ni namna anavyojipambanua kutekeleza kwa vitendo sera ya utawala bora ambayo licha ya kuwa nzuri na yenye lengo la kuongeza uwajibikaji, kwa muda mrefu imekuwa wimbo ambao hauna utekelezaji kwa vitendo.
"Kwa kweli Mh, Rais Samia amenigusa sana anachokifanya huo ndio utawala bora na tunamuombea mungu, aendeleze na utararatibu huo kwani utaongeza uwajibikaji kwa wanaopewa majukumu na sisi chama cha wazee Wanaume Tanzania tunamuunga mkono na pia tungewaomba watanzania tumuunge mkono na tumpe ushirikiano.
Hilo
suala la utawala bora ndilo ambalo tunalipigia kelele muda mrefu sana,kwamba
mtu akifanya kosa awajibike mwenyewe ama awajibishwe na sio
kubadilishiwa nafasi wakati kwa sasa Tanzania hatuna uhaba wa watendaji wala wataalam,hivyo
hakuna sababu kabisa ya kuwakumbatia wasiotaka kuwajibika na hili likisimamiwa
vizuri,ufanisi utaongezeka kwani kila mmoja,atakuwa makini.
Sisi
tunamwambia Mh Rais akaze uzi kwani kila kitu kiko wazi,na kila mmoja anajua
wajibu wake,wala asimuangalie mtu usoni,mtu yeyote anayekwenda kinyume na
taratibu,awajibishwe kwa manufaa ya nchi yetu."alisema Bw.Mwamaji.
Hatua ya Mh Dr.Rais Samia Suluhu Hassan ya kuonyesha kwa vitendo utekelezaji wa utawala bora pia ikazungumziwa na baadhi ya wastaafu wataalam akiwemo Bw.Michael Kingazi ambaye ni mtaalam wa afya mstaafu, yeye pamoja na kuungana na wengine kuongeza Rais Dr Samia,ameshauri suala la uwajibikaji na kuwawajibisha wasiofuata maelekezo zifanyike kwa wote wanaofanya makosa yakiwemo ya kushindwa kusimamia taasisi na idara walizopewa na kwamba kipimo Cha kiongozi kufanikiwa ama kutofanikiwa kiwe ni matokeo ya idara na taasisi wanazoziongoza.
"Hakuna kosa dogo yote ni makosa na tukifumbia macho makosa madogo ndio yanaozaa makosa makubwa,hata vitabu vya mungu vinasema hakuna dhambi ndogo na kubwa zote ni dhambi tu"alisema Kingazi.
Miongoni mwa majukumu makubwa ya chama Cha wazee Wanaume Tanzania (CCWWT) ni pamoja na
kushirikiana na Wadau wengine ikiwemo Serikali kukemea vitendo vya ukatili
vinavyoendelea kushika kasi katika jamii,kukabiliana na mmomonyoko wa maadili
katika jamii sambamba na kutoa elimu ya athari zake.
MWISHO.
Comments
Post a Comment