BENK YA CRDB YAENDELEA KUPASUA ANGA KIMATAIFA, SASA YABISHA HODI MAREKANI.


 

Benk ya CRDB imeendelea kuwa kinara wa kujenga mtandao mkubwa wa huduma za kifedha  kitaifa na  kimataifa  baada  ya  kuingia makubaliano  ya ushirikiano  katika utoaji  wa huduma na Benki ya kimataifa ya American Express  ya nchini  Marekani.

Katika  makubaliano hayo wateja wa Benk ya American Expres  na  wale  wa Benk ya CRDB  watakuwa na  kadi  ambayo itaweza  kutumika  kwenye mashine za ATM za benk zote mbili  popote Duniani .

Akizungumza wakati  wa hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Benk ya CRDB Bw Abdul Majid Nsekela  amesema hatua hiyo  itapunguza gharama na pia  mzigo wa kutembea na fedha fursa ambayo  itawanufaisha  hasa wanapokuja kutalii nchini.


Kwa upande wake mwakilishi wa Benk hiyo ambaye pia ni  Makamu wa Rais wa American Express anayewakilisha nchi za Ulaya, Mashariki ya Kati na pia Afrika  Bi Briana Wilsey amesema kutokana  na mtandao  mkubwa  wa Benk hiyo kote duniani usirikiano  huo utakuwa na  tija  kubwa katika  nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania na  ameipongeza Benk ya  CRDB kwa kuwa miongoni  mwa Benk zinazokua  kwa  kasi  na zenya  mtandao  mkubwa kaika  ukanda  wa  Afrika  mashariki..


 

Akizungumza  baada ya uzinduzi huo mkuu wa mkoa wa Arusha Bw.John Mongela amesema hayo ni mafanikio makubwa na  ni  matokeo ya kazi  kubwa inayofanywa na serikali  ya Tanzania  chini ya Mh,Rais  Dr  Samia Suluhu  Hassani ya kuimarisha  sekta ya utalii.

 

Watendaji  wa Benk ya  CRDB akiwemo makamu mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Benk hiyo  Profesa Neema Mori  amesema  wanajivunia mafaniko makubwa ya Benk hiyo  ambayo ni matokeo ya kazi  nzuri na kubwa wanayoendelea  kuifanya  ya  kuimarisha utoaji  wa huduma.



Baadhi  ya  wadau wa utalii wameipongeza Benk ya CRDB kwa hatua  iliyofikiaambapo  kwa sasa  inatoa  huduma  katika nchi mbalimbali  za Afrika  Mashariki  ikiwemo   Burundi na Kongo.

Kwa Habari zaidi  usikose kutembelea    AMTV upate  habari  kwa  kina.

Comments

Popular posts from this blog

TAMKO LA KULAANI MAUAJI......CHAMA CHA WAZEE WANAUME TANZANIA (CCWWT)CHALAANI MAUAJI YA KIKATILI YA MTOTO MKOANI KAGERA

WAZIR PEMBE ATAKA UZINGATIAJI AFYA YA AKILI

VIONGOZI CHAMA CHA WAZEE WANAUME TANZANIA (CCWWT) WAPAZA SAUTI JUU YA HATUA ANAZOCHUKUA RAIS DR SAMIA