ARUSHA TRADE FAIR KUSHIRIKIANA NA TIGO KUTOA HUDUMA KWA GHARAMA NAFUU WAKATI WA SIKUKUU ZA MWISHO WA MWAKA 2023

 


KAMPUNI ya Bulb Africa LTD imeandaa maonyesho maalum kwa ajili  ya  wajasiriamali na wafanyabiashara kwa ujumla   yanayojulikana kwa jina la  Arusha Trade Fair yanayofanyika katika  viwanja vya Azimio Jijini  Arusha

Mratibu  wa  maonyesho  hayo  Bw  Agustino  Namfua  amesema  Jumla ya wafanyabiashara na wajasiriamili 150 wanatarajia kushiriki  na yataanza tarehe 12-17  mwezi Disemba  2023

 Augustine Namfua ametaja baadhi  ya  fursa  za  Maonesho hayo kuwa ni Pamoja  na kuwawezesha  wananchi wa Arusha kujipatia mahitaji, huduma na bidhaa mbalimbali kwa ajili ya sikukuu za krismas na mwaka mpya kwa Bei rafiki.

Katika Kongamano hilo pia mada mbalimbali zitawasilishwa na wataalamu ikiwemo ya namna ya kunufaika na  Mikopo, uwekezaji na huduma za kifedha.


 Wadhamini  wakuu  wa  Kongamano  hilo  ni  kampuni  ya simu za  mkononi ya  Tigo ambayo Meneja wake wa kanda ya kasikazini Bw  Daniel Mainoya amesema kuwa wao kama kampuni ya mawasiliano wanafuraha kuwawezesha wafanyabiashara na wajasiriamali kutumia huduma Bora za tigopesa kuuza na kununua bidhaa kwa urahisi.

Amesema pamoja na Huduma za keep fedha pia katika Banda lao watakuwa wakiuza simu na vifaa vingine vya mawasiliano kwa Bei nzuri inayoendana na kampeni ya zawadi dabodabo.

KWA HABARI  ZAIDI  ,USIKOSE  TEMBELEA   AMTV UZIPATE KWA  UNDANI  NA  KWA  KINA


Comments

Popular posts from this blog

TAMKO LA KULAANI MAUAJI......CHAMA CHA WAZEE WANAUME TANZANIA (CCWWT)CHALAANI MAUAJI YA KIKATILI YA MTOTO MKOANI KAGERA

VIONGOZI CHAMA CHA WAZEE WANAUME TANZANIA (CCWWT) WAPAZA SAUTI JUU YA HATUA ANAZOCHUKUA RAIS DR SAMIA

TAMWA-ZANZIBAR YATOA RAI WAKATI WA UANDAAJI SERA, SHERIA