WATAFITI NA WAHADHIRI WA VYUO NCHI ZA SADC WAVUNJA UKIMYA,UTUPAJI OVYO WA TAKA
WATAFITI na wahadhiri wa vyuo vikuu kutoka nchi 4 (nne) kati ya (kumi na sita )16 za SADC wamekutana jijini Arusha kujadili namna ya kukabiliana na athari za utupaji ovyo wa taka katika mimea na viumbehai wakiwemo wanyamapori kuptia mradi unaotekelezwa na SADC kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Jumuiya ya Ulaya .
Mwakilishi wa Sekretarieti ya SADC anayesimamia Rasilimali Dr. Geoge Wambura amesema mradi huo unatarajiwa kuwa na tija kubwa kwani miongoni mwa wadau wanaoutekeleza ni wataalam waliobobea kwenye sekta ya utafiti wakiwemo wahadhiri wa vyuo vikuu
Miongoni mwa vyuo vinavyoshiriki katika utekelezaji wa mradi huo ni pamoja na chuo cha utafiti na usimamizi wa wanyamapri Afrika cha Mweka , ambapo mkuu wa chuo hicho Profesa Jafari Kideghesho amesema jukumu kubwa kwao ni kusimamia utafiti na kuandaa mitaala ya kufundishia itakayotumika kwa nchi zote za SADC .
Mr Brian Halubanza .mwakilishi kutoka Zambia
Prof Alexs Kisingo mwakilishi kutoka Tanzania
Dr Kwaslema Male .Mratibu wa Mradi kutoka Tanzania
ILI UPATE TAARIFA KWA UNDANI ZAIDI WALICHOSEMA WATAALAM HAWA , TEMBELEA .....AMTV
UPATE HABARI KWA KINA NA KWA UNDANI ZAIDI
Comments
Post a Comment