WAZUNGUMZAJI WA LUGHA ISIYOFUNGAMANA NA TAIFA LOLOTE DUNIANI KUKUTANA ARUSHA
Mkutano wa kimataifa wa watu wanaodaiwa kuzungumza Lugha inayoitwa Esperanto wanatarajiwa kukutana Arusha katika mkutano wao unaotarajiwa kufanyika mwezi Augost mwaka huu 2024
Mkurugenzi wa kituo cha kimataoifa cha mikutano cha Arusha Bw Epraim Mafuru amesema watu zaidi ya 1.000 kutoka mataifa zaidi ya 100 wanaozungumza lugha isiyo na asiyoufungamana na Taifa lolote Duniani wanatarajiwa kukutana Arusha kujadili namna lugha hiyo inavyoweza kuyaunganisha mataifa yote Duniani .
Mmoja wa wanachama
wa Lugha hiyo iliyopewa jina la
Lugha ya ESPERANTO Bw Francis Gendo amesema hii ni mara ya kwanza kwa wadau
wa Luga hiyo ambayo
kwa sasa inazungumzwa na watu
zaidi ya milioni tano kote Duniani kukutana katika nchi ya Tanzania na Bara la
Afrika kwa ujumla
Tayari Kamati ya maandalizi ya mkutano huo imeshakamilisha hatua za awali za kuwezesha wazungumzaji wa lugha hiyo kukutana ikiwa ni Pamoja na kukamilisha taraatibu zote za kiserikali kitaifa na kimataifa zinazohitajika.
Kwa mujibu wa wadau hao, Esperanto ni Lugha ambayo haina
asili na taifa lolote duniani, na haifungamani na Lugha yeyote Duniani hivyo
mtu yeyote anaweza kujifunza na kuitumia na wanasema imeanza kupata wafuasi
wengi wakiwemo wasio na lugha za asili
Comments
Post a Comment