WAZUNGUMZAJI WA LUGHA ISIYOFUNGAMANA NA TAIFA LOLOTE DUNIANI KUKUTANA ARUSHA

Mkutano wa kimataifa wa watu wanaodaiwa kuzungumza Lugha inayoitwa Esperanto wanatarajiwa kukutana Arusha katika mkutano wao unaotarajiwa kufanyika mwezi Augost mwaka huu 2024 Mkurugenzi wa kituo cha kimataoifa cha mikutano cha Arusha Bw Epraim Mafuru amesema watu zaidi ya 1.000 kutoka mataifa zaidi ya 100 wanaozungumza lugha isiyo na asiyoufungamana na Taifa lolote Duniani wanatarajiwa kukutana Arusha kujadili namna lugha hiyo inavyoweza kuyaunganisha mataifa yote Duniani . Mmoja wa wanachama wa Lugha hiyo iliyopewa jina la Lugha ya ESPERANTO Bw Francis Gendo amesema hii ni mara ya kwanza kwa wadau wa Luga hiyo ambayo kwa sasa inazungumzwa na watu zaidi ya milioni tano kote Duniani kukutana katika nchi ya Tanzania na Bara la Afrika kwa ujumla Tayari Kamati ya maandalizi ya mkutano huo imeshakamilisha hatua za awali za ...