UTUNZAJI WA MAZINGIRA WAANZA KULETA TIJA WILAYANI LONGIGO KUPITIA BIASHARA YA HEWA UKAA

Wananchi wa vijiji 16 vya wilaya ya Longido mkoani Arusha wamesaini makubaliano ya kuanza kunufaika na hewa ukaa kati yao na wawekezaji wa kampuni Soil for the Future Tanzania yanayoashiria wananchi hao kuanza kunufaika na hewa ukaa baada ya kuhifadhi mazingira ambayo yameanza kuwavutia wawekezaji hao wa rasilimali hiyo . Wakizungumzia hatua hiyo viongozi na watendaji wa vijiji hivyo wamesema tayari wameshaingia makubaliano ya awali ya miaka mitano na wawekezaji hao mbapo kila kijiji kitapata asilimia 51 ya mapato yatokanayo na hewa ukaa kila mwaka. Hata hivyo wananchi hao akiwemo Bw Simion Olotosoi amewataka wawekezaji hao kuheshimu makubaliano kwani uz...