WANACHAMA WAMCHAGUA TENA MLAY KUWA RAIS MCT

NA HAJI NASSOR, ARUSHA WANACHAMA wa Baraza la Habari Tanzania MCT, wamemrejesha tena Rais wa Baraza hilo, Jaji Mstaafu: Juxon Isaac Mlay kwa miaka mengine mitatu ijayo, kupitia mkutano mkuu wa 25, uliofanyika Septemba 28, 2023 mkoani Arusha. Mkutano huo, pia umemchagua Yussauf Khamis Yussuf kuwa Makamu wa rais na wingine waliochaguliwa katika mkutano huo ni wawakilishi wa vyombo vya habari, akiwemo Tido Mhando. Wawakilishi wingine ni Rose Rouben, Ali Haji Mwadini samba mba na kupatikana kwa wawakilishi watatu, kundi la umma wakiongozwa na CPA: Happiness Nkya, Jaji Robert Makaramba na Mwajaa Said. Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo, rais aliyerejea tena madarakani Juxon Isaac Mlay, alisema kasi na ari iliyokuwepo kwa miaka mitatu, ni vyema ikaongezeka. Aliwataka viongozi wenzake, waliorudi kutetea nafasi zao, kuhakikisha wanaendelea kufanya makubwa, wakiwa ndani ya Baraza la Habari Tanzania, ili kuwalipa wanachama waliowachagua. ‘’Niwaombe wale viongo...