WANACHAMA WAMCHAGUA TENA MLAY KUWA RAIS MCT
NA HAJI NASSOR, ARUSHA
WANACHAMA wa Baraza la Habari Tanzania MCT, wamemrejesha tena Rais wa Baraza hilo, Jaji Mstaafu: Juxon Isaac Mlay kwa miaka mengine mitatu ijayo, kupitia mkutano mkuu wa 25, uliofanyika Septemba 28, 2023 mkoani Arusha.
Mkutano huo, pia umemchagua Yussauf Khamis Yussuf kuwa Makamu wa rais na wingine waliochaguliwa katika mkutano huo ni wawakilishi wa vyombo vya habari, akiwemo Tido Mhando.
Wawakilishi wingine ni Rose Rouben, Ali Haji Mwadini samba mba na kupatikana kwa wawakilishi watatu, kundi la umma wakiongozwa na CPA: Happiness Nkya, Jaji Robert Makaramba na Mwajaa Said.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo, rais aliyerejea tena madarakani Juxon Isaac Mlay, alisema kasi na ari iliyokuwepo kwa miaka mitatu, ni vyema ikaongezeka.
Aliwataka viongozi wenzake, waliorudi kutetea nafasi zao, kuhakikisha wanaendelea kufanya makubwa, wakiwa ndani ya Baraza la Habari Tanzania, ili kuwalipa wanachama waliowachagua.
‘’Niwaombe wale viongozi wenzangu, tuliochaguliwa kuhakikisha tunafufua ari na kasi mpya, ili kuendelea kulipatia maendeleo endelevu na wanachama wake Baraza letu,’’alieleza.
Katika hatua nyingine, Rais huyo wa Baraza la Habari Tanzania alimtangaaza Ernest Sungura, kuwa ndie anayetarajiwa kubeba mikoba ya nafasi ya Katibu Mtendaji mpya.
‘’Kwani miezi mitatu ijayo, Katibu Mtendaji wa sasa Kajubi Mukajanga, anatarajiwa kustaafu, hivyo tayari Bodi ya wadhamini imeshamteua mtu, wa kushika nafasi hiyo,’’alieleza.
Katibu Mtendaji wa MCT anayemaliza muda wake Kajubi Mukajanga, alisema anajivunia umoja na mshikamano, aliyoupata kutoka kwa wafanyakazi wenzake, katika kipindi cha utumishi wake.
Aidha alisema, sasa anashukuru, wakati anamaliza muda wake, tayari MCT inayofisi, na huku vyombo vya habari na waandishi wake, wakiwa wamepata uwelewa wa mambo kadhaa.
‘’Lakini kubwa zaidi, ni kuendelea kufanikisha uwepo wa utamaduni wa mashindano ya umahiri wa waandishi wa habari, kwa miaka 14 mfululuzo sasa,’’alieleza.
Hata hivyo Katibu huyo Mtendaji, alieleza kuwa, anaendelea kusononeshwa na wanachama wa MCT, wasiolipa ada zao, akisema wanadhofisha baadhi ya harakati za kimaendeleo.
Akiwasilisha ripoti ya utendaji ya MCT, Afisa kutoka baraza hilo Saumu Mwalimu, alisema kwenye ufuatiliaji wao wa vyombo vya habari, wamegundua vyombo vya habari vya magazeti, vimekuwa vikijibebesha kazi ya kutoa hukumu, kwenye vichwa vyao vya habari.
‘’Kwa mfano, vipo vichwa vya habari vinavyoandikwa na wahariri, hutoa jawabu au hukumu kwa aina habari iliyoripotiwa, lakini na kuendesha mazungumzo yasio na tija kwa watangaazaji wa redio,’’anaeleza.
Nae Afisa wa MCT Paul Mallimbo, alisema wanachofanya baada ya kuona chombo cha habari, kinakengeuka kanuni, sheria na sera za uandishi wa habari, ni kuviandikia barua.
Wakichangia ripoti za fedha na za utendaji, washiriki wa mkutano huo akiwemo Jabir Idrissa, alilipongeza Baraza kwa kazi kubwa wanazozifanya, hasa za utatuzi wa migogoro.
Mwandishi Nevile Meena, alisema kama waandishi wa habari hawafanyi habari za uchambuzi wanaweza kuachwa nyuma na wasiosomea uandishi wa habari.
Wakati huo huo, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Kajubi Mukajanga, alisema, bado kuna uminywaji wa habari, na kuwakosesha taarifa wananchi, kujua kinachoendelea serikali.
Katib huyo Mtendaji, alitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari, ukumbi wa Kibo, jengo la Mahkama ya Afrika, mkoani Arusha ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya kujua duniani.
Alisema ujumbe wa mwaka huu, wa unakwenda sambamba na kauli ya Waziri mkuu wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaaliwa Kassim Maajaliwa.
‘’Ujumbe wa mwaka huu unaosema ‘umuhimu wa matumizi ya mitandao ya kijamii katika kupata taarifa’ jambo ambalo linakwenda samba mba na sheria kadhaa za habari,’’alieleza.
Kwa upande wake Mhadhiri wa Chuo cha Kiislamu Murorogo, Rehema Twahiri, alisisitiza umoja na mshikamano wa vitendo baina ya waandishi wa chombo kimoja na chingine,’’alishauri.
Ne Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria Tanzania ‘OUT’ Vicent Mpepo, alisema hata kama vyanzo watu vya kutoa habari, ifikiriwe namna kwa MCT.Z2/
atika mkutano huo mkuu wa 25 wa Baraza la Habari Tanzania MCT, ulihudhuria na wanachama hai 54, kati ya 61 ambao hawana deniAAAA hadi mwaka 2023.
Mwisho
Comments
Post a Comment