KAMANDA MCHOMVU AWAPA NENO WAZAZI

KAMANDA  wa polisi Mkoa wa Mjini Magharibi kamishina Msaidizi wa Polisi Richard (ACP), Thadei Mchomvu, amewataka wazazi na walezi  kushirikiana kwa pamoja katika kuwalea na kuwatunza watoto wao kwa ajili ya kuwalinda   na vitendo vya ukatili na udhalilishaji.

Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili ofisini kwake Muembe Madema Mjini Zanzibar, amesema baadhi ya wazazi  hushughulikia  shughuli zao zaidi na hawana utamaduni wa  kuwa  karibu na watoto wao jambo ambalo hupelekea kuendelea vitendo hivyo.

"Wapo wazazi wakitoka asubuhi ndo wametoka kurudi kwao ni usiku watoto wakiwa wamelala, mtindo ambao unachangia watoto kukosa elimu ya kujitambua  iliyo muhimu katika kuwasaidia kuepuka kufanyiwa vitendo viovu vya kudhalilishwa," alisema Richard

" Na baadhi ya kina mama wanawacha watoto kudhurura ovyo bila ya kuwavisha nguo kamili na kupelekea mtoto kufanyiwa vitendo vya ukatili na udhalilishaji." Aliongezea Richard

Aidha alisema kuna faida mbalimbali zinazopatikana wazazi wakishirikiana kwa pamoja katika kumlea watoto wao.

"Ushirikiano wa wazazi katika malezi ya mtoto huwezesha kugawana majukumu na mzigo wa kumlea mtoto. Hii inamaanisha kuwa mzazi mmoja hatakuwa na jukumu kubwa la kumlea mtoto peke yake, na hivyo kupunguza shinikizo na mafadhaiko ya mzazi mmoja, ushirikiano wa wazazi unaweza kuongeza uhusiano mzuri na mawasiliano kati yao, ambayo ni muhimu katika kujenga familia yenye furaha na imara".alisema Richard

"Faida nyingine ya wazazi kushirikiana katika malezi ni kwamba inawezesha mtoto kupata upendo na huduma kutoka kwa wote wawili. Mtoto anapopata upendo na huduma kutoka kwa wazazi wote, anajenga uhusiano wa karibu na wote wawili na hivyo kuimarisha hisia za usalama na utulivu. "aliongezea Richard

Pia alisema takriban  asilimia 80% ya matukio  ya ubakaji ambayo yamehusisha mabinti chini ya miaka  kumi na mmoj 11 hadi kumi na saba 17.

“Jumla ya matukio ya kubakaji 285,katika matukio hayo watoto wenye umri 0-10 walikuwa 30,mabinti kuanzia miaka 11hadi 17 walikuwa 232,  na wasichana kuanzia miaka 18 na kuendelea walikuwa ni 23." alisema Richard.

 

Comments

Popular posts from this blog

TAMKO LA KULAANI MAUAJI......CHAMA CHA WAZEE WANAUME TANZANIA (CCWWT)CHALAANI MAUAJI YA KIKATILI YA MTOTO MKOANI KAGERA

VIONGOZI CHAMA CHA WAZEE WANAUME TANZANIA (CCWWT) WAPAZA SAUTI JUU YA HATUA ANAZOCHUKUA RAIS DR SAMIA

TAMWA-ZANZIBAR YATOA RAI WAKATI WA UANDAAJI SERA, SHERIA