Posts

TAMKO LA KULAANI MAUAJI......CHAMA CHA WAZEE WANAUME TANZANIA (CCWWT)CHALAANI MAUAJI YA KIKATILI YA MTOTO MKOANI KAGERA

Image
  TAMKO LA (CCWWT) KULAANI   MAUAJI   YA KIKATILI   YA   MTOTO   ASIMWE .   Chama cha wazee   wanaume Tanzaniaa   (CCWWT)kimeungana   na   Rais Mh Dr Samia Suluhu Hassan na wadau   wengine   kulaani kitendo cha kuuawa kikatili   kwa Mtoto   Asimwe   Novati   mwenye ulemavu wa Ngozi (Albino) akiwa na umri wa miaka miwili na nusu yaliyotokea kijiji cha Gulamula Wilaya ya Muleba Mkoa wa Kagera Akitoa tamko hilo   kwa niaba ya chama   k iongozi mkuu   wa chama hicho Bw Tadey Mchena amesema wanachama   wa chama cha wazee   wanaume kimesikitishwa   sana na ukatili   huo aliofanyiwa mtoto huyo na kuendelea   kusisitiza umuhimu wa   hatua kalia   za   kisheria   kuchukuliwa kwa   waliohusika. Aidha   kwa   mujibu wa Bw Mchena chama cha   wazee   wanaume Tanzania   kiko   tayari kutoa ushirikiano wa hali na mali ...

WAZUNGUMZAJI WA LUGHA ISIYOFUNGAMANA NA TAIFA LOLOTE DUNIANI KUKUTANA ARUSHA

Image
Mkutano  wa kimataifa wa watu wanaodaiwa kuzungumza Lugha inayoitwa   Esperanto wanatarajiwa kukutana Arusha katika mkutano wao unaotarajiwa kufanyika mwezi Augost   mwaka   huu 2024 Mkurugenzi wa kituo cha kimataoifa cha mikutano cha Arusha Bw Epraim Mafuru amesema watu zaidi ya 1.000 kutoka  mataifa   zaidi   ya 100   wanaozungumza lugha isiyo na asiyoufungamana   na Taifa   lolote Duniani   wanatarajiwa kukutana   Arusha kujadili namna lugha hiyo   inavyoweza kuyaunganisha mataifa yote Duniani .  Mmoja wa   wanachama wa Lugha hiyo   iliyopewa   jina la   Lugha ya ESPERANTO Bw Francis Gendo amesema hii ni mara ya kwanza   kwa wadau   wa Luga   hiyo   ambayo   kwa   sasa inazungumzwa na watu zaidi ya milioni tano kote Duniani kukutana katika nchi ya Tanzania na Bara la Afrika kwa ujumla Tayari Kamati ya maandalizi ya mkutano huo imeshakamilisha hatua za awali za ...

WANANCHI WANAOISHI JIRANI NA HIFADHI WATOBOA SIRI NZITO YA KUSHAMIRI KWA MIGOGORO KATI YAO NA WATENDAJI WA HIFADHI

Image
  Hivi karibuni mgogoro  wa  muda mrefu kati ya  wananchi  wa Kijiji cha Bugeri kilichoko wilayani  Karatu mkoani  Arusha na Hifadhi ya Taifa  ya  Ziwa  Manyara ulipata ufumbuzi baada ya serikali kuamua kumega eneo la ukubwa wa hekari nane (8) na kuligawa kwa wananchi waliokuwa wamelivamia , Taarifa ya uamuzi huo ilitolewa na mkuu  wa mkoa  wa Arusha Bw  John Mongela katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijjini hapo ambapo pia alitumia nafasi hiyo  kutoa  msimamo wa serikali. Kikao hicho pia kiliwashirikisha watendaji wa hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara akiwemo mkuu wa hifadhi hiyo Kamishna wa Uhifadhi Eva Malya ambaye alielezea mchakato waliopitia hadi kufikia hatua. pia  walikuwepo wataalam wa ardhi mkoa  wa Arusha walioongozwa na Mpima wa mkoa  Bw Dany Mruma ambaye alitoa  ufafanuzi wa kitaalam juu ya masuala ya mipaka na sheria zinazotumika. baada ya maamuzi hayo wananchi nao wakapata naf...

WATAFITI NA WAHADHIRI WA VYUO NCHI ZA SADC WAVUNJA UKIMYA,UTUPAJI OVYO WA TAKA

Image
  WATAFITI na wahadhiri  wa vyuo vikuu kutoka nchi  4 (nne) kati ya (kumi na sita )16 za SADC wamekutana jijini  Arusha kujadili namna ya kukabiliana na athari  za utupaji ovyo wa taka katika mimea na viumbehai wakiwemo wanyamapori kuptia mradi unaotekelezwa  na SADC kwa  kushirikiana na  wadau  mbalimbali ikiwemo  Jumuiya ya  Ulaya . Mwakilishi  wa  Sekretarieti  ya  SADC  anayesimamia  Rasilimali Dr. Geoge  Wambura amesema mradi  huo unatarajiwa  kuwa na tija  kubwa kwani  miongoni mwa  wadau wanaoutekeleza ni  wataalam waliobobea  kwenye  sekta ya utafiti wakiwemo  wahadhiri wa  vyuo  vikuu Miongoni  mwa  vyuo  vinavyoshiriki katika utekelezaji  wa  mradi  huo ni pamoja na chuo  cha utafiti na  usimamizi wa wanyamapri  Afrika  cha  Mweka , ambapo   mkuu  wa chuo  hich...

UTUNZAJI WA MAZINGIRA WAANZA KULETA TIJA WILAYANI LONGIGO KUPITIA BIASHARA YA HEWA UKAA

Image
  Wananchi   wa    vijiji   16   vya wilaya   ya Longido mkoani   Arusha wamesaini makubaliano ya kuanza kunufaika na hewa ukaa kati yao na wawekezaji   wa kampuni Soil for the Future Tanzania  yanayoashiria   wananchi   hao kuanza   kunufaika   na   hewa ukaa   baada   ya   kuhifadhi mazingira   ambayo   yameanza   kuwavutia   wawekezaji hao wa   rasilimali   hiyo . Wakizungumzia hatua hiyo viongozi na watendaji  wa vijiji  hivyo   wamesema tayari  wameshaingia  makubaliano  ya  awali ya miaka mitano  na wawekezaji  hao mbapo  kila  kijiji  kitapata  asilimia  51  ya  mapato  yatokanayo na hewa  ukaa  kila  mwaka.  Hata hivyo   wananchi   hao   akiwemo Bw Simion Olotosoi    amewataka   wawekezaji hao kuheshimu makubaliano kwani uz...

ARUSHA TRADE FAIR KUSHIRIKIANA NA TIGO KUTOA HUDUMA KWA GHARAMA NAFUU WAKATI WA SIKUKUU ZA MWISHO WA MWAKA 2023

Image
  KAMPUNI ya Bulb Africa LTD imeandaa maonyesho maalum kwa ajili   ya   wajasiriamali na wafanyabiashara kwa ujumla     yanayojulikana kwa jina la   Arusha Trade Fair yanayofanyika katika   viwanja vya Azimio Jijini   Arusha Mratibu   wa   maonyesho   hayo   Bw   Agustino   Namfua   amesema   Jumla ya wafanyabiashara na wajasiriamili 150 wanatarajia kushiriki   na yataanza tarehe 12-17   mwezi Disemba   2023   Augustine Namfua ametaja baadhi   ya   fursa   za   Maonesho hayo kuwa ni Pamoja   na kuwawezesha   wananchi wa Arusha kujipatia mahitaji, huduma na bidhaa mbalimbali kwa ajili ya sikukuu za krismas na mwaka mpya kwa Bei rafiki. Katika Kongamano hilo pia mada mbalimbali zitawasilishwa na wataalamu ikiwemo ya namna ya kunufaika na   Mikopo, uwekezaji na huduma za kifedha.   Wadhamini   wakuu   wa   Kongamano   hilo ...

BENK YA CRDB YAENDELEA KUPASUA ANGA KIMATAIFA, SASA YABISHA HODI MAREKANI.

Image
  Benk ya CRDB imeendelea kuwa kinara wa kujenga mtandao mkubwa wa huduma za kifedha   kitaifa na   kimataifa   baada   ya   kuingia makubaliano  ya ushirikiano   katika utoaji   wa huduma na Benki ya kimataifa ya American Express   ya nchini   Marekani. Katika   makubaliano hayo wateja wa Benk ya American Expres   na   wale   wa Benk ya CRDB   watakuwa na   kadi   ambayo itaweza   kutumika   kwenye mashine za ATM za benk zote mbili   popote Duniani . Akizungumza wakati   wa   hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Benk ya CRDB Bw Abdul Majid Nsekela   amesema hatua hiyo   itapunguza gharama na pia   mzigo wa kutembea na fedha fursa ambayo   itawanufaisha   hasa wanapokuja kutalii nchini. Kwa upande wake mwakilishi wa Benk hiyo ambaye pia ni  Makamu wa Rais wa American Express anayewakilisha nchi za Ulaya, Mashariki ya Kati ...